Thursday, February 17, 2011

Three Secrets to Happiness 
 
 
 
 
 
 
_,_._,___

Thursday, February 10, 2011

Laazizi

 1. Mapenzi kitu ajabu, yakutia bumbuwazi
  Yakufanya uwe bubu, kujibu huwa huwezi
  Shubiri kwako zabibu, na vitamu huviwezi.
 2. Wamkuta kaemewa, asemayo hayajuwi
  Aumba akiumbuwa, aona maruwiruwi
  Vigumu kumuopowa, na kwa ngisi kumvuwi.
 3. Hukumbuka ya zamani, yote walofanyiana
  Nyumbani barabarani, ayaona kama jana
  Akili yake ya nyani, aruka inagongana.
 4. Wangoja nyota ya jaha, kutwa wewe unahaha
  Mawazo yako silaha, akukwaaye usaha
  Usifanyiwe msaha, waugeuza karaha.
 5. Kalelewa kaleleka, utani kwake ni mwiko
  Njiani yeye na kaka, hapokei mualiko
  Ghadhabu zake za paka, hapendi maziko.
Hashil S. Hashil

Aushi ya bin-a-dam

Maisha ya binadamu ni kitu ambacho hakijatiliwa maanani abadan katan. Insi wengi ulimwenguni wanachukulia jambo hili kama sadfa tu. Sie sote twaishi kwa aushi ya kuomba. kuna mambo mengi sana ambayo yanamfinyilia mwanadamu chini. Baadhi yao ikiwa:
1. Pesa.
2.Mume ama mke.
3.Vijulanga.